Tuesday, October 13, 2015

MAREHEMU AAMKA KABLA YA UPASUAJI

Hospitali
Wahudumu katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini Mumbai walipigwa na butwaa baada ya mwanamume kuamka muda mfupi kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Daktari mkuu alikuwa amesema mwanamume huyo wa miaka 50 alikuwa amefariki na akaagiza mwili wake upelekwe mochwari mara moja.
Agizo hilo lilikiuka kanuni za hospitali kwani watu wanaotangazwa kufariki hutakiwa kukaa kwenye wadi saa mbili, kuhakikisha hakuna kosa na ni kweli wamefariki dunia.
Madaktari wanasema mwanamume huyo kwa jina Prakash alikuwa na matatizo ya mwili kuendesha shughuli za kawaida na alikuwa akiropokwa alipofikishwa hospitalini.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema alipatikana katika kituo cha mabasi akiwa amepoteza fahamu.
Akiongea katika kikao cha wanahabari Jumatatu, Dkt Suleman Merchant, anayesimamia hospitali ya Lokmanya Tilak alisema Prakash ni mlevi “aliyejitelekeza” na alikuwa na mabuu usoni na masikioni.
"Miili ya wafu kawaida ndiyo huwa na mabuu. Lazima alikuwa amekaa pahali amelala siku sita au saba,” alisema daktari Merchant.
Aliambia wanahabari kwamba daktari aliyemchunguza Prakash alimpima mpigo wa moyo, mpigo wa damu na hata kupumua kwake.
Dkt Merchant amesema hospitali hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Prakash yuko katika hali thabiti hospitalini ambako anaendelea kutibiwa.

Tags:
Unknown About Unknown

Hii ni blog kwaajili ya kukupa habari za kila aina ulimwenguni ili usiweze kupitwa na jambo habari mpya,michezo,burudani,sanaa,nyimbo mpya,video@Nuru fm Newsroom/production
View all posts by admin →

Get Updates

Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

Share This Post

0 comments:

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Nuru fm Iringa Enhanced by Joseph Martin

© 2015 NURU FM. NURU FM JOSEPH Y. converted by NURU FM NEWSROOM
Powered by Blogger.