Jimbo la Arusha Mjini limekuwa Jimbo la
tatu kuahirisha Uchaguzi wa Wabunge baada ya baadhi ya Wagombea na
nafasi hiyo kufariki muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwa Jimbo hilo, Mgombea mmoja aliyekuwa akipeperusha Bendera ya ACT-Wazalendo, Estomih MALLAH alifariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi na kukimbizwa Hospitali.
Marehemu Estomih tayari ameagwa na kufanyiwa ibada katika Kanisa la KKKT Ngulelo, leo October 14 2015 Marehemu anasindikizwa na ndugu, jamaa pamoja na watu wengine kwenda Kijijini kwao eneo la Sango Mkoa wa Kilimanjaro ambako yatafanyika mazishi.
Apumzike kwa amani Marehemu Mzee ESTOMIH MALLAH… #RIP
0 comments: