.

.
All Stories

Wednesday, October 14, 2015

http://www.riverside.courts.ca.gov/gavel.jpg
Dodoma. Mtayarishaji wa vipindi, Sospiter Jonas amefikishwa katika
Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma Mjini akishtakiwa kwa matumizi mabaya ya
mtandao.

Sospiter alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mussa
mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Emmanuel Bwile.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook ujumbe
kuwa “Pinda utakuwa muhubiri wa injili tu.”

Mussa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alibandika picha ya John
Maliga kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika ujumbe huo, kitendo
ambacho ni kinyume cha kifungu namba 16 cha Sheria ya Mtandao ya Mwaka 2015.

Mlalamikaji katika shauri hilo la jinai namba 815/2015 litakalokuja tena
mahakamani Oktoba 19, ni John Maliga.

Mshtakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyomtaka kuwa
na mdhamini mmoja na bondi ya Sh1 milioni.

Kesi hii imekuja baada ya wiki iliyopita, kijana mmoja, Benedict
Ngonyani (24) kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam akituhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange.

Kijana huyo anatuhumiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook na
WhatsApp kuwa, Mwamunyange, amelazwa kwenye hospitali moja mjini
Nairobi, Kenya kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.
Unknown         No comments:

unnamed V
Jimbo la Arusha Mjini limekuwa Jimbo la tatu kuahirisha Uchaguzi wa Wabunge baada ya baadhi ya Wagombea na nafasi hiyo kufariki muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwa Jimbo hilo, Mgombea mmoja aliyekuwa akipeperusha Bendera ya ACT-WazalendoEstomih MALLAH alifariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi na kukimbizwa Hospitali.
Marehemu Estomih tayari ameagwa na kufanyiwa ibada katika Kanisa la KKKT Ngulelo, leo October 14 2015 Marehemu anasindikizwa na ndugu, jamaa pamoja na watu wengine kwenda Kijijini kwao eneo la Sango Mkoa wa Kilimanjaro ambako yatafanyika mazishi.
unnamed II

unnamed
unnamed IV
unnamed V
Apumzike kwa amani Marehemu Mzee ESTOMIH MALLAH… #RIP
Unknown         No comments:
http://www.ghanaplaylist.com/assets/coverart/14448030415801_0.jpeg
Safari hii Fally pupa kamtafuta 2face Idibia kutoka Nigeria na wameamua kuifanya hii track iitwayo Sweet life rmx.
Unknown         No comments:

Tuesday, October 13, 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza na wanahabari juu ya mambo yahusuyo tume hiyo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia mfumo mpya wa kielektroniki katika kujumlisha matokeo ya kura kwa lengo la kuondoa makosa mbalimbali ya kibinadamu, yanayoweza kutokea kwa bahati mbaya wakati wa kujumlisha matokeo hayo katika uchaguzi mkuu.
Mfumo huo mpya wa Menejimenti ya Matokeo (RMS), unatumia mashine za kisasa zenye uwezo wa kuchapisha na kunukushi karatasi za kupigia kura zaidi ya 60 kwa dakika moja.
Mkurugenzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema jana kwamba Oktoba 11, mwaka huu, waliwaalika wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kutoka vyama vyote vya siasa na mfumo huo ukapitishwa.
Akiwasilisha mada ya maandalizi ya uchaguzi, Kombwey alitaja makosa yanayoweza kutokea katika kujumlisha kura ni pamoja na matokeo ya kituo kimoja, kujumlishwa zaidi ya mara mbili, kukosea uandikaji wa namba na usahihi wa ujumlishaji.
“Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 mfumo huu ulisanifiwa upya na kutumika, hata hivyo kasoro chache zilioneshwa. Kwa uchaguzi wa mwaka huu, tume imeboresha mfumo huu na kuondoa upungufu katika maeneo yote yaliyokuwa na changamoto mwaka 2010,” alisisitiza Kombwey.
Alisema pamoja na mfumo huo, pia tume hiyo imeandaa mfumo mbadala, alioutaja kuwa ni Spreadsheet Excel RMS, ambao utatumika iwapo kutakuwa na changamoto katika kutumia mfumo uliondaliwa.
Aidha alisema tume hiyo inafanya maandalizi ya kutumia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa ajili ya kutuma matokeo yote, badala ya kutumia mtandao wa simu za mkononi. “Katika uchaguzi wa mwaka 2010, utumaji wa matokeo ulikuwa na changamoto nyingi. Kati ya majimbo 239 ni majimbo 150 tu yaliweza kutuma matokeo kwa mfumo uliokuwa umeandaliwa, ambao ni kupitia mtandao wa simu za mikononi, matokeo yaliyobaki yalitumwa kwa nukushi ,” alifafanua.
Alisema kitendo cha kutumia mkongo huo wa taifa, kitasaidia upatikanaji wa matokeo mapema kama inavyokusudiwa, ingawa pia njia mbadala ya kutuma matokeo kwa nukushi imeandaliwa na halmashauri zote zimepatiwa vifaa, vitakavyowezesha utumaji wa matokeo kwa haraka kufanyika.
Aidha, tume imekubaliana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhusu kutumia Mkongo wa Mawasiliano wa Tamisemi, kusaidia utumaji wa taarifa za matokeo kutoka katika halmashauri hadi NEC. Kuhusu elimu, Kombwey alisema jumla ya asasi za kiraia 451 ziliomba kutoa elimu ya mpiga kura.
Kati ya hizo ni asasi 447 zilikidhi vigezo na hivyo kupewa kibali cha kutoa elimu hiyo. Alisema asasi hizo zimesaini Maadili ya Utoaji wa elimu ya Mpiga kura na kukubali kutumia mwongozo wa Elimu ya Mpiga kura.
Unknown         No comments:
Rais Jakaya Kikwete akitembelea mradi wa kufua umeme kutokana na gesi asilia baada ya kuzindua mradi huo Kinyerezi Dar es Salaam jana. (Picha na Freddy Maro).
Rais Jakaya Kikwete amezindua kituo cha kufua umeme kwa mitambo ya gesi asilia cha Kinyerezi I na kutaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuchangamkia fursa ya upungufu wa umeme Afrika ili kuwa na uhakika wa mapato.
Alisema duniani umeme unaozalishwa ni megawati milioni 5,255,000 na mataifa makubwa matano yanazalisha asilimia 55 wa megawati hizo, ambayo ni China inaongoza kwa megawati milioni 1,146,000, Marekani milioni 139,000, Japan 287,000, Urusi 223,000 na India 280,000.
Alisema megawati zinazobakia, ndiyo nchi nyingine 193 zinazotambulika na Umoja wa Mataifa wanagawana, ambapo Afrika zinazalishwa megawati 111,786, idadi ambayo hata nusu ya India haifikii.
Alisema Afrika Kusini wanaongoza kwa kuzalisha megawati 44,260, Misri megawati 26,910, Algeria megawati 11,330, Libya megawati 6,763, Morocco megawati 6,620 na Nigeria megawati 5,600.
Rais Kikwete alisema katika nchi za Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa megawati 2,465, Tanzania 1,498, Uganda megawati 850, Rwanda megawati 110 na Burundi megawati 53, hali inayoonesha kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme.
“Lakini kwa kuwa nchi yetu imejaliwa vyanzo vingi vya nishati ni fursa na kugeuza kuwa biashara, kwani Kenya wanahitaji megawati 1,000, Rwanda, Zambia na wengineo wanataka kwa haraka huku wengine wakitaka kujenga bomba la kupeleka gesi wenyewe,” alisema.
Alisema kwa sasa nchi inapita kwenye changamoto, kwani umeme wa maji unaingiza megawati 561 katika gridi ya taifa, lakini sasa zinazoingia ni megawati 105 na upungufu ni megawati 450.
Alisema alitegemea kutakuwa na vituo zaidi kuzalisha umeme, kwani bomba lina uwezo wa kusafirisha gesi kutengeneza megawati 3,000, lakini bado kuna nafasi kufikia malengo kwa kujenga haraka vituo vingine.
Alisema katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaokamilika mwakani mwishoni, lengo ni kufikisha megawati 2,780, lakini sasa kuna megawati 1,490, hivyo kudaiwa megawati 1,390. Alisisitiza kwamba jitihada zinahitajika kufikisha hizo mwakani.
Alisema baada ya kukamilika Kinyerezi I, mwezi ujao itakamilika Kinyerezi II na Januari mwakani Kinyerezi III, hivyo ni lazima kuongeza kasi. Kikwete aliwataka Tanesco kuongeza kasi ili kuchangamkia fursa na kuingiza umeme haraka na kupunguza mgao uliopo sasa.
Alisisitiza shirika hilo la umeme kuzingatia sheria ya manunuzi kwa umma. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava alisema katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, vituo vya kufua umeme vya megawati 484.8 vimejengwa na pia asilimia 47 ya mitambo ya kufua umeme imejengwa .
Alisema, miradi mingi ya kufua, kusafirisha na kusambaza umeme inaendelea na ujenzi. Alisema tangu Septemba 17 mwaka huu, walipoanza kuwasha mitambo ya gesi asilia, wameongeza megawati 200 ambazo hazikuwepo kabla ya gesi kuanza kusafirishwa, vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi, kwani kungekuwa na ukosefu wa megawati 400.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema kituo hicho kimoja, kati ya vinne vinavyojengwa, vikikamilika , vina uwezo wa kutoa megawati 1,500. Kituo cha Kinyerezi I kimegharimu Sh bilioni 400.
“Kwa sasa mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha megawati 70 ndiyo imeishajaribiwa na tayari inazalisha umeme na miwili iliyobaki ina jumla ya megawati 80 itaanza kujaribiwa na itakamilishwa na kuunganishwa mwisho wa mwezi huu,” alisema.
Unknown         No comments:
Hospitali
Wahudumu katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini Mumbai walipigwa na butwaa baada ya mwanamume kuamka muda mfupi kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Daktari mkuu alikuwa amesema mwanamume huyo wa miaka 50 alikuwa amefariki na akaagiza mwili wake upelekwe mochwari mara moja.
Agizo hilo lilikiuka kanuni za hospitali kwani watu wanaotangazwa kufariki hutakiwa kukaa kwenye wadi saa mbili, kuhakikisha hakuna kosa na ni kweli wamefariki dunia.
Madaktari wanasema mwanamume huyo kwa jina Prakash alikuwa na matatizo ya mwili kuendesha shughuli za kawaida na alikuwa akiropokwa alipofikishwa hospitalini.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema alipatikana katika kituo cha mabasi akiwa amepoteza fahamu.
Akiongea katika kikao cha wanahabari Jumatatu, Dkt Suleman Merchant, anayesimamia hospitali ya Lokmanya Tilak alisema Prakash ni mlevi “aliyejitelekeza” na alikuwa na mabuu usoni na masikioni.
"Miili ya wafu kawaida ndiyo huwa na mabuu. Lazima alikuwa amekaa pahali amelala siku sita au saba,” alisema daktari Merchant.
Aliambia wanahabari kwamba daktari aliyemchunguza Prakash alimpima mpigo wa moyo, mpigo wa damu na hata kupumua kwake.
Dkt Merchant amesema hospitali hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Prakash yuko katika hali thabiti hospitalini ambako anaendelea kutibiwa.
Unknown         No comments:
Kwa kawaida panya akionekana machoni pa mwanadamu anauawa ama hata kutegwa na kupewa sumu lakini sio hawa panya wa Sokoine.
Unknown         No comments:
© 2015 NURU FM. NURU FM JOSEPH Y. converted by NURU FM NEWSROOM
Powered by Blogger.